Monday 2 June 2014

Leo nataka kuongea kuhusu wasanii na uchoyo walionao katika nyanja hii ya burudani.Mara nyingi wasanii huitana na kueka vikao bila kujua kuwa pana watu ambao wanahitajika kwenye vikao hivyo kuboresha mazungumzo.Naongelea kuhusu Ma Djs ambao wanapiga mziki na wanajua kwa sasa ni mziki aina gani upo masikioni na ni vipi msanii anaweza toka.Jamaani wasanii hawa Ma DJs ni muhimu sana hebu msiwadharau wapeni nafasi muone.

Thursday 4 April 2013

Wimbo wa klean heart wawacha wachovu mdomo wazi

Klean heart ni msanii wa kizazi kipya anaetokea mji wa Malindi pwani ya Kenya. Amekuwa kwa safu ya mziki miaka kadhaa hivi huku akiwa na kibarua cha kuufanya mziki wa malindi upande ngazi za kimataifa. Amewahi kushinda tuzo kadha ikiwemo ile ya Uhuru live concert iliyodhaminiwa na shirika la mawasiliano Celtel kenya. Kwa sasa amewachilia video hii ya nyimbo kinaya aliyomshirikisha Jix ambayo inaonekana kama alikuwa akiwadadisi wasanii fulani, Japo sio wengi wenye kuielewa nyimbo hii lakini inaonekana kama kejeli flanii hivi.Klean heart anapanga kusafiri Nairobi kukamilisha album yake.

Thursday 28 February 2013

klean heart - chemchem za kisanii Official video


Dorothy Nyambu a.k.a Dotty akanusha kile ambacho wenzake wanakieneza kuwa mchumba wake anamzuia kuendeleza talanta yake.Anasema amekuwa na mwito mkubwa kwenye safu hii ya filamu na kila mmoja anataka aende mbele hata mchumba wake pia.Dotty ambaye aliwahi onekana kwa mara ya kwanza katika filamu ya MUME NI KAZI iliyotayarishwa na Ogutu Atata chini ya Heartland kenya,anashukuru familia yake kumpa support kubwa na tayari anatayarisha filamu nyingine kwa jina UZITO WA HISIA ambayo ananuia kufanya vizuri zaidi."nimejifunza mengi hasa wakati tukiwa kwenye mazoezi na sasa naja na mbwembwe za hali ya juu"asema Dotty